MPANGO WA KUKUZA UCHUMI-GMDF UMOJA PILE Karibu katika umoja wa GMDF UMOJA PILE. Umoja wa GMDF UMOJA PILE umepata hati ya usajili kisheria kutoa huduma ndogo za fedha kwa wanachama wake. Lengo kuu la umoja huu ni kujenga uwezo wa kiuchumi kwa wanachama wake kwa pamoja kwa kushirikiana pamoja. Kujifunza uwekezaji, elimu ya fedha na kuweka akiba kwa mwanachama na kwa kwa wanachame kupitia umoja huu. Walengwa wa umoja huu. Walengwa wakuu wa kikundi hiki ni watu wote lakini zaidi mtu yeyote anayetaka kujifunza maarifa mapya hasa elimu ya fedha, elimu ya uwekezaji na kuweka akiba Mtu ambaye anataka au anatamani kuanza kujifunza kujitegemea mwenyewe na kuajiri wengine sasa au baadaye Mwenye biashara ambaye anatamani kukua kibiashara, kuongeza ujuzi, kukuza mtaji wake na kujifunza njia mpya ya kuongeza thamani ya bidhaa na kuwa na ubora. Mfanyakazi ambaye ameajiriwa na ambaye anataka kuongeza ujuzi katika uwekezaji na kujifunza biashara na uwekekezaji. Mwanafunzi wa chuo na yule ambaye amehitimu (graduants) bado anatafuta ajira umoja huu ni muhimu kujifunza na kufikia malengo. Taasisi au ngo's pia anaweza kujiunga na kuwa mwanachama Familia moja au watu wa karibu (marafiki) wanaweza kuwa wanachama wa umoja huu. Umoja huu unawawaunganisha ndugu kwa pamoja Jinsi ya kujisajiri na kuwa mwanachama wa GMDF UMOJA PILE Kujisajiri kwa kujaza taarifa za msingi katika mfumo na kulipa ada ya uanachama au kujaza taarifa kupitia fomu za uanachama ambazo zinapatikana kwa Kiongozi Mwanachama. Ada ya uanachama ni ths 35,000/= kwa mwaka (Non-refundable) Kwa taarifa zaidi juu ya umoja huduma zake tembelea www.gmdf.or.tz na kisha tembelea ukurasa wa GMDF UMOJA kwa maelezo Zaidi. Kwa mawasiliano au kutaka kujua zaidi wasiliana nasi GMDF UMOJA PILE, SLP 80256, Temeke Pile,Dar es salaam0755-089-5450677-356-714